Padre richard a. Mjigwa, c. Pp. S jubilei ya miaka 25 ya daraja takatifu ya upadre 2024 - | vatican news

Padre richard a. Mjigwa, c. Pp. S jubilei ya miaka 25 ya daraja takatifu ya upadre 2024 - | vatican news


Vaticannews is ON AIR - VIEW NOW

Please note: this is Beta feature.


Play all audios:

Loading...

Katika mahubiri yake Padre Tumaini Ngonyani Litereku alikazia umuhimu wa kuwa na moyo wa shukrani, furaha na unyenyekevu na kwamba, Padre awe ni sababu ya furaha ya watu wa Mungu, kama


ilivyokuwa kwa Kristo Yesu, Mtumishi wa furaha. Unyenyekevu ni siri ya mafanikio katika maisha; ni kuyakubali makuu ya Mungu, tayari kuyatumia kunogesha furaha ya watu wa Mungu kwa


kuhakikisha kwamba, anatumia vyema karama na mapaji aliyokirimiwa na Mungu. NA PADRE PHILEMON ANTHONY CHACHA, SDB., - VATICAN. Mapadre wanapaswa kuwa ni mfano na kielelezo cha Kristo Yesu


Mchungaji mwema, kwani wanapaswa kujisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya Kristo Yesu na Kanisa lake; sadaka inayojionesha katika mchakato wa maisha na utume wa Kipadre, kwa kujikita


katika huduma makini kwa Familia ya Mungu wanayoihudumia. Waamini wanatambua na kuthamini sadaka ya maisha ya Mapadre wanaojitosa bila ya kujibakiza; wahudumu wa Mafumbo ya Kanisa


wanaotekeleza dhamana na wito wao katika hali ya unyenyekevu pasi na makuu. Mara nyingi hawa ni viongozi wanaoonesha dira na njia ya kufuatwa wala si watu wanaotoa amri na kuendelea “kuponda


maisha.” Mapadre wanaojisadaka barabara ni mfano mwema katika maisha ya kiroho na wengi wanaweza kuwatambua Mapadre wa namna hii kuwa kweli ni “Watu wa Mungu” ambao hawajamezwa na


malimwengu na kutopea huko huko! Jumamosi tarehe 27 aprili 2024 katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Paolo, Roma nchini Italia zilitawala shwange na nderemo kwa watanzania waishio nchini humo.


Hii ilikuwa ni kusheherekea Jubilei ya miaka 25 ya Daraja Takatifu ya Upadre ya Padre Richard, Mjigwa C.PP.S., wa Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu. Padre Richard Mjigwa maarufu


kama “Mtoto wa Mkulima: Falsafa ya Ufagio ni Unyenyekevu” alizaliwa tarehe 28 Novemba 1964, Makoko, Parokia ya Nyamiongo Jimbo Katoliki la Musoma. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre


na Kitawa, tarehe 17 Aprili 1999, Askofu Msaidizi Cesare Nosiglia wa Jimbo Katoliki la Roma, akampatia Daraja Takatifu ya Upadre kwenye Parolia ya “Corpo e Sangue di Gesù” Jimbo kuu la


Roma. Padre Mjigwa akiwa kwenye picha ya pamoja na watawa walioshiriki Misa Takatifu. SHEREHE ZA KUMPONGEZA BABA RICHARD HAPA ROMA ZILIANZA NA IBADA YA MISA TAKATIFU YA KUMSHUKURU MUNGU KWA


ZAWADI YA JUBILEI YA MIAKA 25, HUKU PADRE RICHARD MWENYEWE AKIWA NDIYE mwadhimishaji Mkuu wa Misa. Pembeni mwake alikuwepo Padre Paulo Kaigarula aliyezaliwa tarehe 18 Februari1970. Aliweka


nadhiri za muda 10 Septemba 1995 na za daima tarehe 9 Desemba 1998. Alipewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 12 Septemba 1999 nchini Italia. Huyu ndiye Mkarmeli wa kwanza mtanzania, ambaye


na yeye anasherehekea Jubilei ya Miaka 25 ya Upadre. Alikuwepo pia Padre Felix Mushobozi, C.PP.S., Katibu mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu kanda ya Tanzania. Padre


Emmanuel Tumaini, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Wakatoliki Italia, JWWI, na Padre Tumaini Ngonyani Litereku, maarufu kama “Baba Lite.” ambaye alikuwa Mhubiri katika Ibada hii ya Misa


Takatifu. Pamoja nao walikuwepo mapadre wengi, Shemasi, Watawa, Waseminari, wageni kutoka Tanzania ambao walikuwepo hapa Roma kwa ajili ya kufanya Hija, Sigfried Filipo Nnembuka, mwakilishi


wa Balozi wa Tanzania nchini Italia, ndugu pamoja na maafisa wengine wa Ubalozi. Mapadre walioshiriki katika Ibada ya Misa Takatifu, Jubilei ya Miaka 25 ya Upadre KATIKA MAHUBIRI YAKE PADRE


TUMAINI NGONYANI LITEREKU ALIKAZIA UMUHIMU WA KUWA NA MOYO WA SHUKRANI, FURAHA NA UNYENYEKEVU NA KWAMBA, PADRE AWE NI SABABU YA FURAHA YA WATU WA Mungu, kama ilivyokuwa kwa Kristo Yesu,


Mtumishi wa furaha. Unyenyekevu ni siri ya mafanikio katika maisha; ni kuyakubali makuu ya Mungu, tayari kuyatumia kunogesha furaha ya watu wa Mungu. Padre Lite alianza kwa kusema kuwa


katika sherehe ambazo aliwahi kufurahi sana, basi moja wapo ni hii, ambayo ni kubwa ikifuata ile ya upadre wake. Padre Litereku alisisitiza katika neno Furaha, akijiliuza Furaha ile ya kweli


inatoka wapi? Aliendelea kwa kusema mfano wa Furaha ni Yesu Kristo ambae pia ni Mtumishi wa furaha yetu. Huku akiendelea kutafuta chimbuko la furaha hii, aliweza kuunganisha na Injili


aliyoichagua, ikiwa ni ile ya Yesu kuwaponywa wakoma kumi (Lk 17,11-19). Wakoma hawa walitengwa kwa jinsi walivyokuwa na hivyo kukosa ile furaha kwasababu walijiona kama watu ambao


hawatambuliki, lakini walikuwa na matumaini kuwa siku moja watapata ile furaha ya kuponywa ule ugonjwa wao. Hivyo kukutana kwao na Yesu sala yao ilikuwa “Bwana utuonee Huruma” kwa sala hiyo


ni ishara wazi kuwa walikuwa wanaomba kuponywa. Lakini Yesu anawaabia waende wakajionyeshe kwa makuhani. Lakini walipokuwa njiani mmoja wao aliposikia ameponywa anageuka kwa moyo wa shukrani


na furaha anageuka kumshukuru Mungu. Padre anapaswa kuwa ni chemchemi ya furaha kwa watu wa Mungu PADRE TUMAINI ANAENDELEA KWA KUSEMA: “YESU KRISTO MTUMISHI WA FURAHA YETU ANAPOTUTENDEA


MAKUU ANATUONESHA KWANZA YEYE MWENYEWE JINSI ALIVYO: hana kikomo, anajishusha, anawagusa, anawaponya na baadaye anawatuma, enenda imani yako imekuponya”. Kumbe, Yesu Kristo anategemea


unyeyekevu kutoka kwetu kama ilivyo falasafa ya ufagio ya Baba Mjigwa. Hivyo tukitakaswa na kuwezeshwa katika maisha yetu, na kama tunahitaji kuwa na mafanikio zaidi, ni lazima kuwa na


unyenyekevu. Unyenyekevu kwa maana ya kukubali makuu ya Mungu ambayo ametujalia na kuyatumikia kwa furaha. Kumbe, tunaitwa hata sisi kwenda kutangaza na kuwa sababu ya hii furaha kwa


wenzetu. Padre Litereku alimalizia kwa kumpongeza sana Padre Mjigwa pamoja na kuahidi kumwombea na kumshukuru Mungu kwa zawadi hii ya Wito wa Upadre. Amemsihi aendelee kuwa na moyo wa furaha


siku zote, aendelee kuwa na moyo wa sala, moyo wa shukrani na unyenyekevu, ili daima furaha yake izidi kuwa kubwa zaidi na kuenea kwa watu wengi zaidi, hasa wale wanaomsikiliza katika


vipindi mbalimbali vya Radio Vaticani, Idhaa ya Kiswahili. Padre Mjigwa akifungua zawadi aliyokabidhiwa na watanzania NAYE PADRE RICHARD MJIGWA, C.PP.S., KATIKA KUSHEHEREKEA JUBILEI HII


ANASEMA: “MIAKA 25 YA DARAJA TAKATIFU YA UPADRE NI ZAWADI, NI DHAMANA, NI UTUME NA WAJIBU AMBAO MWENYEZI MUNGU amenikabidhi kuutenda na kuhushuhudia kwa watu wa Mataifa”. Itakumbukwa kuwa


katika miaka hii 25, Padre Richard Mjigwa amewahi kuwa Paroko Usu kwa miaka 3 Parokia ya Mtongani, Kunduchi Jimbokuu la Dar es Salaam; Muasisi na Mhariri Mkuu Radio Mwangaza FM, Dodoma; Mkuu


wa Chuo cha Ufundi cha Mtakatifu Gaspari, Kunduchi, Jimbo Kuu la Dar es Salaam; Mwandishi na Mtangazaji wa Radio Vatican, Roma, nchini Italia Hakika Padre Mjigwa katika miaka hii amepitia


changamoto nyingi, yeye mwenyewe anasema kati ya changamoto hizo ni kutetereka kwa afya ambako aligundulika kuwa alikuwa na tatizo katika utumbo mnene na hivyo ilipelekea kufanyiwa


operesheni ya dharura mwaka 2011 na aliweza kupona huku madaktari wakiwa wanashangaa kwa sababu ni tatizo kubwa lililokuwa linapelekea kifo. Baba Mjigwa alipoulizwa nini ushauri anaoweza


kutoa hasa katika siku hii muhimu katika maisha na utume wake alisema: “pale unapoitwa jitoe kwa akili yako, kwa moyo wako wote na ujue ni hapo hapo tu Mwenyezi Mungu amekupangia na kama


atakuhamisha umshukuru”. Aliongezea “katika maisha na utume wa wito wa aina yeyote ile jitahidi kuwekeza kwa watu, jitahidi kujenga mahusiano na mafungamano mema na watu na hao watakusaidia


katika maisha na utume wako, na kamwe hutatindikiwa na lolote.”  Tunaposherehekea na kumpongeza Padre Richard Mjigwa, C.PP.S., tunaalikwa kila mmoja wetu kumwombea ili aweze kuwa mwaminifu


na mwadilifu katika wito, maisha na utume wake.  Jubilei ya Miaka 25