Mchango na sadaka ya ijumaa kuu 2023: nchi takatifu, siria na uturuki: majanga na vita - | vatican news

Mchango na sadaka ya ijumaa kuu 2023: nchi takatifu, siria na uturuki: majanga na vita - | vatican news


Vaticannews is ON AIR - VIEW NOW

Please note: this is Beta feature.


Play all audios:

Loading...

Mchango na sadaka ya Ijumaa kuu kwa Mwaka 2023 ni kwa ajili ya Nchi Takatifu, Siria na Uturuki nchi ambazo zimeathirika sana kutoka na tetemeko la ardhi lililojitokeza hivi karibuni, kiasi


cha kufisha juhudi kubwa za maboresho ya maisha ya watu wa Mungu baada ya janga kubwa la Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19.. Hii ni fursa ya moja kwa moja kwa waamini kuwa ni mashuhuda


na vyombo vya: haki, amani na huruma sanjari na kuendeleza maeneo matakatifu. NA PADRE RICHARD A. MJIGWA, C.PP.S. – VATICAN. Mchango na Sadaka ya Ijumaa kwa Ajili ya Nchi Takatifu ni fursa


ya moja kwa moja kwa watu wa Mungu sehemu mbalimballi za dunia kuwa ni mashuhuda na vyombo haki, amani na maridhiano kati ya watu. Msaada huu ni ishara ya umoja na ushiriki katika utume wa


Mama Kanisa katika mchakato wa kulinda na kuendeleza  maeneo Matakatifu. Mchango na sadaka hii inayotolewa na waamini, kila Ijumaa kuu ni kiungo muhimu sana kwa Wakristo wanaoishi katika


Nchi Takatifu. Mtakatifu Paulo VI, kwa mara ya kwanza katika historia ya Kanisa, alitembelea Nchi Takatifu mwezi Januari 1964 na kuguswa na mahitaji ya Wakristo. Katika Wosia wake wa Kitume


“Nobis in animo” yaani “Umuhimu wa Kanisa katika Nchi Takatifu” uliochapishwa tarehe 25 Machi 1974, alikazia umoja na mshikamano wa waamini. Huo ukawa ni chimbuko la Mchango na Sadaka ya


Ijumaa kuu kwa ajili ya Nchi Takatifu: "Pro Terra Sancta".  Mtakatifu Paulo VI alihimiza sana umuhimu wa uwepo endelevu wa Kanisa katika Nchi Takatifu, kama amana na urithi wa


imani; ushuhuda endelevu wa Jumuiya ya Wakristo unaoonesha jiografia ya ukombozi. Tangu wakati huo, Kanisa linaendelea kuwakumbuka na kuwaombea Wakristo pamoja na watu wote wenye mapenzi


mema, wanaoteseka kunyanyaswa na hata kuuwawa huko Mashariki ya Kati, lakini hasa kutokana na imani yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake. Mchango wa Ijumaa Kuu 2023: Nchi Takatifu, Uturuki na


Siria   (AFP or licensors) SADAKA NA MCHANGO WA IJUMAA KUU KUTOKA KWA MAKANISA YOTE DUNIANI, NI ALAMA YA UPENDO, UDUGU NA MSHIKAMANO WA KANISA KWA WATU WA MUNGU WANAOISHI KATIKA NCHI


TAKATIFU. Huu ni ushuhuda wa mchakato wa majadiliano ya kiekumene yanayosimikwa katika uekumene wa damu, huduma na sala pamoja na kuendeleza majadiliano ya kidini ili kujenga na kudumisha


udugu wa kibinadamu katika misingi ya: haki, amani na maridhiano. Ni kwa njia ya ushuhuda wa umoja, upendo na mshikamano Kanisa linataka kuwajengea waamini na watu wote wenye mapenzi huko


Mashariki ya kati Injili ya amani na matumaini ya leo na kesho iliyo bora zaidi ili kuondokana na: vita, vitendo vya kigaidi, misimamo mikali ya kiimani, dhuluma na nyanyaso kwa misingi ya


kidini. Mchango na sadaka ya Ijumaa kuu kwa Mwaka 2023 ni kwa ajili ya Nchi Takatifu, Siria na Uturuki nchi ambazo zimeathirika sana kutoka na tetemeko la ardhi lililojitokeza hivi karibuni,


kiasi cha kufisha juhudi kubwa za maboresho ya maisha ya watu wa Mungu baada ya janga kubwa la Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 kusababisha madhara makubwa kwa maisha ya watu wengi.


Madhara ya vita ambayo imedumu nchini Siria pamoja na tetemeko la ardhi, yamekuwa ni matukio ambayo yameendelea kuzalisha wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji, pamoja na watu wasiokuwa na


makazi ya kudumu. Ni wakati wa ujenzi wa ushuhuda wa upendo na mshikamano MAMA KANISA ANAWAKUMBUKA WOTE HAWA KAMA SEHEMU YA MAISHA YA KANISA LINALOPITIA NJIA YA MATESO KUELEKEA YERUSALEMU


MPYA: “Via Dolorosa.” Mama Kanisa ameendelea kuwa mstari wa mbele kulinda, kutunza na kuyahudumia maeneo takatifu, sanjari na kuendelea kuwasaidia wakristo wanaoishi katika Nchi Takatifu


kuwa ni mashuhuda na vyombo vya Ufufuko kwa kuendelea kuishi katika Nchi Takatifu, mahali alipozaliwa, akaishi, akateswa, akafa na kufufuka Kristo Yesu. Msaada huu ni muhimu sana katika


kuwahudumia wakimbizi, wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum. Fedha hii inatumika pia kwa ajili ya kugharimia miradi ya elimu, afya na ustawi wa jamii, wagonjwa na wazee. Katika


maadhimisho ya Juma Kuu, Baba Mtakatifu anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuonesha upendo na mshikamano wa dhati kwa watu wa Mungu wanaoishi nchi Takatifu, wakitambua


kwamba, kila mmoja wao ni jiwe muhimu sana katika ujenzi wa maisha ya kiroho. Waamini waendelee kuwa ni vyombo na mashuhuda wa Habari Njema ya Wokovu kwa kuhakikisha kwamba, familia, jumuiya


ndogo ndogo za Kikristo, vigango na parokia zao zinakuwa ni mahali pa sala, upendo na udugu wa kibinadamu, kwa kurutubishwa na Neno la Mungu sanjari na ukarimu wa Kiinjili, kwa ajili ya


kulinda, kutunza na kuboresha maeneo matakatifu. Mchango wa Ijumaa kuu   Tafakari ya Kardinali Cantalamess 31 Machi 2023